ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: January 11th, 2021

Kumekuwa na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza nchini Tanzania kama ugonjwa wa kisukari,presha,pamoja na ajali

Ugonjwa wa kisukari na presha ni magonjwa yanayoonekana kuwatesa watu wengi kwasasa ulimwenguni, huku aina ya maisha tunayoishi ndiyo sababu hasa ya ongezeko la magonjwa,mfano kukosa mazoezi na vyakula vyenye mafuta.

Akizungumza ofisini kwake Dr Faith Kundi  ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa amesema ongezeko la ugonjwa wa kisukari ni kubadilika kwa mfumo wa aina ya maisha,kukosa mazoezi,ongezeko la uzito,unywaji wa pombe kupitiliza,kuongezeka kwa umri husababisha kinga mwili kupungua.

Dr FAITH amesema kuna dalili za awali za kisukari mfano kukojoa mara kwa mara,kupata kiu mara kwa mara,kupata njaa mara kwa mara,kuckoka,kupungua uzito na kupata maambukizi ya mara kwa mara mfano UTI na kuwashwa kwa wanawake.

Dr Faith anasema kuna madhara mengine pia ukiwa na kisukari unaweza kupata, kiharusi,upofu wa macho na masikio kuuma na kuziba mishipa ya damu na kuleta presha,mishipa ya fahamu katika tumbo kupata ganzi na kusababisha tatizo la haja kubwa na tumbo kujaa gesi pamoja na kuhara mara kwa mara,na figo kushingwa kufanya kazi.

Tatizo la kisukari huleta tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa iwapo sukari itaingia katika mfumo wa uzazi na kumekuwa na ongezeko kwa wanaume kukosa hamu ya tendo la tendo na upande wa wanawake nao wamekuwa wakikosa hamu ya tendo pia

wataalam wanasema ni vyema wanandoa wanaoishi na ugonjwa wa kisukari kufika hospitali ili kupatiwa tiba ya changamoto inayowakuta na kunusuru ndoa zao.

Inashauriwa pia jamii kufanya mazoezi,kula mlo kamili na kuacha pombe kama hatua za kujikinga na ugonjwa wa kisukari