Maadhimisho Ya Siku Ya Wauguzi Duniani Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Iringa.

Posted on: May 12th, 2020

Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Muuguzi Mfawidhi Victoria Ntara, wameadhimisha siku ya wauguzi Duniani kwa kujengeana uwezo kupitia uwasilishaji wa mafunzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kauli mbiu ya wauguzi “wauguzi sauti ya uongozi, uuguzi afya kwa Dunia nzima”. Yaliyotolewa na mwezeshaji (muuguzi taiajali Gidion Gilbert)


Muuguzi mwezeshaji Gidion Gilbert.

Aidha wauguzi waliwasilisha mafunzo mbali mbali ya kujengeana uwezo ikiwa ni pamoja na huduma bora kwa mgonjwa anaekaribia kukata roho, ikiwa inalenga Zaidi katika kupunguza kifo chenye maumivu kwa mgonjwa huyo, ikiwa ni pamoja na kumuandaa mgonjwa huyo kisaikolojia na kiroho kulingana na Imani yake, sambamba na kumuandalia mazingira yaliyo bora ili kupunguza maumivu ya kifo kwa mgonjwa huyo. (mwezeshaji Victoria Ntara)

 

Mwezeshaji muuguzi mfawidhi Victoria Ntara.

Mafunzo mengine yalilenga kujadili Janga la Dunia kwa sasa la homa ya mapafu linalosababishwa na virusi vya corona(Covid-19) katika kujengeana uwezo Zaidi wa kupambana na janga hilo ikiwa ni pamoja na kukumbushana miongozo mbali mbali ya Afya kutoka duniani kote ya jinsi kujikinga, kuzuia maambukizo na namna ya kuwahudumia wagonjwa hao wa corona endapo watapatikana katika hospitali. (muuguzi mwezeshaji Aliamini Tibendelanya)

 Muuguzi mwezeshaji Aliamini Tibendelanya.

Aidha wauguzi hao walishiriki kwa pamoja mijadala mbalimbali ya huduma za kiuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuboresha huduma ndani ya hospitali ili kuwahudumia wagonjwa wetu katika kiwango cha hali ya juu ya huduma zilizo bora kabisa. (wauguzi wote).


 

wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika mjadala.

Sambamba na hayo yote wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa pamoja waliapa kiapo kama alivyoapa Florence Nightingale muasisi wa uuguzi Duniani ambapo hasa kinalenga Zaidi katika uwajibikaji, utoaji huduma bora na utunzaji siri za wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali yetu.

Wauguzi kwa pamoja walimaliza maadhimisho ya siku ya uuguzi Duniani kwa kuwasha mishumaa na kupata kinywaji kwa Pamoja.

ASANTE MUUGUZI.


Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakiapa.