WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE: DKT. AGUSTINE MAHIGA AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA

image description

Thursday 8th, June 2023
@Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa

Mhe; Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mnamo tarehe 05/12/2019 kujionea maendeleo ya hospitali pamoja na kuangalia hali ya usajili wa vizazi na vifo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na watu wazima kuanzia miaka 12. Katika ziara hiyo Mhe.Waziri aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa pamoja na wawakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa -UNICEF ambapo walipokelewa na uongozi wa hospitali wakiongozwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt.Scholastica Malangalila, Katibu wa Afya na Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali.