Msanii Wa Muziki Wa Kizazi Kipya Ali Salehe Omary Kiba Atembelea Na Kugawa Msaada Wa Dawa Na Vifaa Tiba.

image description

Saturday 1st, October 2022
@Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Omary Kiba ametembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mnamo tarehe 20/12/2019 na kutoa msaada wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi M-5,802,700 na kumkabidhi kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ndugu James, akiambatana na mhe mkuu wa wilaya ndugu Richard Kasesela pamoja na kaimu mganga mkuu wa mkoa ndugu Robertson, muwakilishi kutoka kampuni ya maziwa ya Asas pamoja na mmfamasia mkuu kutoka wide spectrum ndugu Ismail Jarufu ambae alisaidia katika kuratibu zoezi la upatikanaji wa dawa hizo, msanii mwenzake anaejulikana kama Tunda Man pamoja na kituo cha televisheni na radio cha Afrika ya mashariki maarufu kama EATV & RADIO.